Tuesday, 11 July 2017
Friday, 7 July 2017
DIAMOND PLATNUMZ AZUNGUMZIA KUHUSU CHIBU BEATS
Baada ya ukimya wa muda mrefu tangu msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz atangaze ujio wa bidhaa zake za headphone ‘Chibu Beats’, msanii huyo ameelezea kinachochelewesha.
Muimbaji huyo ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa bidhaa hizo zimechelewa kutokana na mchakato wa usajili wa jina.
“Katika usajili wa Chibu Beats jina lilileta matatizo kidogo, ilikwamisha hapo kwa sababu neno beats mtu kashalisajili dunia nzima mtu mwingine asilitumie neno la beats, siunajua ni la Dre. Kwa hiyo tunaweka namna nyingine ambayo itakuwa nzuri, zitatoka zimeshakuwa tayari mpaka sampo, tumeshasikiliza ni fresh sound hatari” amesema Diamond
ALIKIBA AFANUA KWA NINI COLABO YA YVONE CHAKACHAKA NA DAVIDO ZINACHELEWA KUTOKA
Kipindi cha nyuma kulikuwa na taarifa za Alikiba kufanya kolabo na Yvonne Chaka Chaka na Davido lakini hadi leo hazijatoka, sasa Alikiba amelizungumzia hilo.
Alikiba na Yvonne Chaka Chaka
Muimbaji huyo wa Bongo Fleva ambaye December mwaka jana alionekana akiwa studio nchini Afrika Kusini na Yvonne Chaka Chaka, ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa kazi na Mwana Mama huyo ilishafanyika ila kuna mipango inaweka sawa kwanza.
“Kiufupi kwamba nyimbo zipo na taratibu tulishafanya kama mlivyoona tupo studio lakini kuna ratiba lazima ziwepo sio tu umefanya halafu unatoa. Kuna mipango tupo nayo tayari na kila nyimbo itatoka kwa muda wake, na wimbo wangu unatoka hivi karibuni siwezi nikasema ni lini,” amesema Alikiba.
Kuhusu kolabo na Davido alisema, “unajua wasanii kama wasanii muda mwingine tunakuwa na maneno ya kuridhisha watu lakini kiukweli hakijafanyika chochote ila plan zipo za kufanya na muda tukiupata tutafanya il sijajua ni lini kwa sabau nyimbo nilizonazo ni nyingi sana,” amesisitiza.
Mwaka 2015 Davido aliwahi kuulizwa kuhusu na kolabo na Alikiba na jibu lake lilikuwa, “I have a song coming out with Alikiba too, that’s gonna be crazy”.
Subscribe to:
Comments (Atom)
MAJOR LAZER & DJ MAPHORISA - PARTICULAR FT WIZKID,NASTY C & ICE PRINCE
https://www.youtube.com/watch?v=Eh-OiegK3tg

